Mshindi wa tatu akipokea kitita cha sh. laki 3.
Mshindi wa pili, Peter George akipokea kitita cha sh. laki 5
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi kitita
cha sh. milioni 1 mshindi wa kwanza wa shindano la Twiti Wazo Jipya
Kuondoa Umaskini, Jilly Gaudence Kyomo katika hafla iliyofanyika jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management and Enterprenuership, Dk.
Donath Olomi. Kulia ni mshindi wa pili, Peter George na mwanafunzi wa
chuo cha CBE, Ludovick Angelino.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo
wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi shindano la Twiti Wazo
Jipya Kuondoa Umaskini jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management and Enterprenuership, Dk. Donath Olomi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
---
Na Mwandishi Wetu
VIJANA
watatu wa jijini Dar es Salaam, wameibuka washindi katika shindano la
Dk. Reginald Mengi la ‘Kutwit’ kuondoa umasikini nchini.
Mshindi
wa kwanza katika shindano hilo lililopewa jina la Twiti Wazo Jipya
Kuondoa Umasikini ni Jilly …. ambaye aliibuka na kitita cha sh milioni
moja, Peter George (sh 500,000) na Ludovick Angelino (300,000).
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika Ofisi
za Makao Makuu ya IPP, Dk. Mengi alisema shindano hilo lina lengo la
kuibua mawazo mapya jinsi ya kupambana na umasikini.
Alisema
washiriki wa shindano hilo lililozinduliwa Mei 13 na washiriki wengi
walijitokeza kuibua mawazo mapya na washiriki watatu ndio walioshinda.
Dk.
Mengi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, alisema mchakato
wa kupata washindi, ulisimamiwa na Kiongozi wa Taasisi ya Chuo cha
Uongozi na Ujasiliamali (IMED), Donath Olomi na jopo lake.
Akizungumza jinsi washindi hao walivyopatikana, Dk. Olomi alisema jumla ya Twits 481 zimepokelewa kati ya Mei 13 hadi 31.
Alisema
vigezo vilivyotumika katika mchakato huo ni wazo lililoeleweka na
kuelezeka kirahisi, lisiwe wazo ambalo limeshasikika mara nyingi na
liwe linaweza kutekelezeka.
Alisema mshindi wa kwanza Jilly alitoa wazo lililosema ‘Tuwe na utamaduni wa kupenda kile tukifanyacho, tukifanya kwa moyo, uadilif, heshima na kujali muda hata kama it’s self employed.
No comments:
Post a Comment