ZIFF
ZIFF
sasa inapokea maombi kutoka kwa watengenezaji filamu Afrika Mashariki
wanaotaka kushiriki katika warsha ya utengenezaji filamu wakati wa ZIFF
mwaka huu..
Wanafunzi
5 (mmoja toka kila nchi ya Afrika Mashariki) watalipiwa safari, malazi
na chakula ili kushiriki kwenye warsha hiyo. Wanafunzi 5 wengine
watajilipia wenyewe.
Mfumo
wa warsha utakuwa ni kufuatilia kikundi cha watengeneza filamu walio
tayari mafundi watakaokuwa wanatengeneza filamu fupi wakati wa ZIFF.
Utengenezaji huu unaitwa Guerilla Filmmaking (yaani filamu chapchap) na
katika siku 6 filamu itapigwa, itahaririwa na kuonyeshwa ZIFF siku ya
mwisho.
Wanaotaka kushiriki kwenye warsha watume maombi yao hivi:
CV fupi.
Maelezo kwa nini wachaguliwe (maneno 1000)
Maombi yatumwe kwa: workshop@ziff.or.tz
Warsha imedhaminiwa na Goethe Institute na GIZ (Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani) na Jumuia ya Africa Mashariki (EAC)
Maelezo pia yako www.ziff.or.tz
No comments:
Post a Comment