Wednesday, June 12, 2013

ORIJINO KOMEDI WASAINI MKATABA MNONO NA NEXUS SOMA HAPA


clip_image003
Kundi la Orijino Komedi linaloongoza nchini kwa vipindi vyake kupitia television imeingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa kushirikiana na Rockstar4000. Mkataba huo unaipa nafasi Orijino Komedi kuwa wasanii wa kwanza wa luninga kufanya kazi na Nexus.Mkuu wa Kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara wa Kampuni ya Rockstar 4000 Bi. Christine Mosha “Seven” akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
Nexus Consulting Agency imenunua haki zote za usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi la hilo la Komedi ambalo kwa miaka kadhaa sasa limekuwa namba moja katika sanaa ya uchekeshaji. Mkataba huu utakuwa kwa ajili ya kusimamia kipindi cha Orijino Komedi kuweza kuendelea kuwa namba 1 Tanzania na pia kupanua utazamwaji wake nje ya mipaka ya Tanzania.
Mkataba wa Orijino Komedi na Nexus umetajwa kuwa ni wa kuanzia miaka miwili mpaka mitano.
"Kushirikiana na Orijino Komedi ni kitu muhimu kwa Nexus kwani siku zote imekuwa ikitamani kufanya kazi kwa karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao kutokana na vipaji vyao vya hali ya juu wanavyovionyesha kundi hilo,' alisema mkurugenzi mkuu wa Nexus, Bobby Bharwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Nexus Consulting Agency Bw. Bobby Bharwani (kushoto)
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' amesema wana furaha kuingia mkataba na kampuni ya Nexus Agency na ROCKSTAR4000 Africa, ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kukidhi haja ya soko. Pia Seki alisisitiza kwamba mkataba huu ni mnono sana na utawafanya kufanya kazi zao vizuri sana.

No comments:

Post a Comment