Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.
Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka
nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart
Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa
kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii
ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.
Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.
“Hoteli
na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa
ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.
Rais
Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na
maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio
huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura
Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle
atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.
“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”
Alisema
katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar
es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika
kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile
ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle
atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.
Wasafiri wa mikoani
Wasafiri
wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama
atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion
Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais
Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa 4.00 asubuhi na kwa
kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na abiria
yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na wakati huo.
No comments:
Post a Comment