JUMLA
ya madaktari sita na wataalamu wawili ,mmoja wa teknolojia na
mwingine wa utawala kutoka Misri wamewasili nchini kwa ajili ya kutoa
huduma ya upasuaji wa tundu ndogo kwenye Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili(MNH) jijini Dare es Salaam.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein
Mwinyi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa
madaktari hao .
“Madaktari
hawa watasaidia kutoa kutoa tiba na kuwafundisha madaktari wetu
utaalamu huu, hivyo ujio wao utasaidia kupunguza gharama za matibabu
kwa wagonjwa wanaotakiwa kwenda nje ya nchi,” alisema Dk. Mwinyi.
Aliongeza
kuwa madakatari hao watakuwepo katika hospitali hiyo kuanzia Juni 10
hadi 15, mwaka huu kwa ajili ya kutoa huduma hizo.
Dk. Mwinyi aliushukuru ujio huo kwa kuwa utasaidia kubadilishana uzoefu na teknolojia na kuboresha afya ya Watanzania.
Kwa
upande wake, Balozi wa Misri nchini Tanzania, Hossam Omar alisema
ujio wa madaktari hao ni kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo
mbili katika sekta hiyo, ambapo watauendeleza katika maeneo mengine ya
sekta hiyo na nyingine.
No comments:
Post a Comment