Wednesday, June 12, 2013

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AMWAGIA MVUA YA MATUSI RAIS KIKWETE...!!


MATUSI ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jakaya Mrisho Kikwete yamewagawa Watanzania  na  kuwafanya  wawe  na  mitazamo  tofauti.


Wapo  wanaomuunga  mkono  Rais  Kagame  na  wapo  pia  wanaompinga  kwa  kauli  yake...
Rais Kagame alimtukana Rais Kiwete kwa kuita ushauri wake kwamba ni ushauri wa kijinga kwa wanyarandwa,awali Rais Kikwete alizishauri nchi za Rwanda na Congo DRC kukutana na kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani.



Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati wa mkutano wa kujadili amani na mpango wa ulinzi nchini Congo DRC uliofanyika katika Makao Makuu ya AU mjini Addis Ababa Ethiopia.



Katika ushauri huo Rais Kikwete alisema kwamba ni vyema Rais Kagame akakaa katika meza ya mazungumzo ya amani na Rais wa Congo DRC Joseph Kabila ili kumaliza tofauti zao badala ya kutumia nguvu ya kijeshi.



“Nimekaa kimya kwa kipindi kirefu na kwa jinsi nilivyoweza kwa sababu nilifikiri kwamba mazungumzo ya kipuuzi yaliyozungumzwa na watu wajinga yamemalizika "alisema Rais Kagame.



Katika hatua nyingine Rais Kagame alisema kwamba ushauri huo wa Rais Kikwete ni sawa na kuwachezea wanyarandwa mbele ya mataifa.  



Rais Kagame aliyasema hayo katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya maofisa wa jeshi wapatao 45 katika kituo cha mafunzo ya kijeshi siku ya Juma Tatu nchini Rwanda.

No comments:

Post a Comment