Zaidi ya Sh100 milioni zinatarajiwa kutumika kugharimia mazishi ya mfanyabiashara, bilionea wa madini ya Tanzanite, Erasto Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi 21 Jumatano ya Agosti 7, mwaka huu.
Kiasi hicho kinachotarajiwa kuchangwa na
wafanyabiashara wenzake wa madini kitatumika pia kulipia gharama za
magari maalumu yatakayotumika kwenye msafara wa mazishi ya Msuya
yanayotarajiwa kufanyika nyumbani kwao Mererani, wilayani Simanjiro.
Habari kutoka kamati ya mazishi inayoundwa na
wafanyabiashara wa Tanzanite, ikiongozwa na kaka mkubwa marehemu Msuya,
Gady Msuya, gari maalumu la kubeba mwili wa marehemu na jeneza
vimeagizwa kutoka Nairobi, nchini Kenya kwa gharama ya Sh8 milioni.
No comments:
Post a Comment