BABA MZAZI APOTEZA FAHAMU MAHAKAMANI.
Baba Mzazi wa Kijana aliye hukumiwa hukumu ya Miaka 30
Jela, Mzee Mohamedi Nzunja akiwa amepoteza fahamu kufuatia Hukumu iliyo tolewa
kwa Mwanae.
Baadhi ya wanafamilia wakifarijiana nje ya Mahakama baada ya ndugu yao kuhukumiwa
Dada wa Kijana aliye hukumiwa kifungo cha Miaka 30 Jela akiwa ameishiwa nguvu nje ya Mahakama
Mzee Mohamed Nzunja katikati akinyanyuliwa na mkwewe ili kupelekwa Hospitali
Baadhi ya wanafamilia wakifarijiana nje ya Mahakama baada ya ndugu yao kuhukumiwa
Dada wa Kijana aliye hukumiwa kifungo cha Miaka 30 Jela akiwa ameishiwa nguvu nje ya Mahakama
Mzee Mohamed Nzunja katikati akinyanyuliwa na mkwewe ili kupelekwa Hospitali
Mahakama ya wilaya ya Mbeya imemuhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Nsalaga Uyole jijini Mbeya baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wa kidato cha pili jina linahifadhiwa Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Nsalaga.
Mwendesha mashitaka wa Serikali Mheshimiwa Lugano Mwakilasa ameiambia mahakamani hiyo kuwa Nizra Mohamed (24) mkazi wa Uyole jijini Mbeya alitenda kosa hilo Novemba 5 mwaka jana (2012) majira ya saa 12 jioni.
Amesema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a 155 sura ya 16 ya marekebisho kanuni ya adhabu mwaka 2002 .
Kwa upande Serikali umeleta ushahidi wake ambao ni Askari walioipeleleza kesi hiyo pamoja na Daktari na binti aliye fanyiwa kitendo hicho
Awali binti huyo ameieleza Mahakamani hiyo kuwa Novemba 5 mwaka jana majira ya saa 12 jioni alivamiwa na mshitakiwa ambaye ni fundi Mwashi Katika eneo la Nsalaga ambapo mshitakiwa huyo alimkamata kwa nguvu na kumpeleka ndani ya nyumba iliyokuwa iaendelea kujengwa (pagara) kisha kumlawiti na kumsababishia maumivu makali hali iliyopelekea kukimbizwa katika hospitali ya mkoa kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo Daktari Satumani aliyemfanyia uchunguzi Binti huyo amethibitisha mbele ya mahakama hiyo kuwa binti huyo alifanyiwa kitendo hicho cha kinyama ambapo alimpa tiba katika hospitali ya Mkoa jijini Mbeya.
Mashahidi wengine akiwemo Askari Polisi amesema kuwa awali mshitakiwa alikili kosa hilo mbele ya kiapo cha Polisi kituo cha kati Mbeya ambapo mara baada ya uchunguzi kukamilika waliifikisha kesi hiyo mahakamani.
Aidha mshitakiwa huyo alileta mashahidi wawili ambao ni mafundi waashi ambao kwa pamoja walieleza mahakama hiyo kuwa hawa kujua nini kinacho endelea mahakamani hapo.
Baada ya mahakama hiyo chini ya hakimu Gilbert Ndeuruo kuridhishwa na ushahidi kwa pande zote mbili ambapo aliamuru mshitakiwa huyo kutumikia kifungo Cha miaka 30 jela ili iwefundisho kwa wengine.
Pamoja na kupatiwa nafasi ya kujitetea mshitakiwa alishindwa kutoa utetezi wake ambapo ilionekana akijikanyaga mahakamani kwa kusema kuwa hakumbuki kama alimlawiti au kumbaka mwanafunzi huyo hali iliyo mpa fursa Hakimu Ndeuruo kutoa adhabu ya miaka 30 Jela.
Hata hivyo ndugu na jamaa wa karibu na mshitakiwa waliangua Vilio na wengine kuzirai akiwepo baba mzazi wa mshitakiwa pia mke wa mshitakiwa aliye kuwa na kichanga hali iliyo pelekea wa huduma wa mahakama kufanya kazi ya kuwa tuliza watu hao.
No comments:
Post a Comment