Wednesday, January 29, 2014
CCM WASHANGAA HELIKOPTA YA CHADEMA
Na Mwandishi wetu, Arusha
Chama cha mapinduzi (CCM)kimesema kuwa kinashangazwa na kitendo cha
chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema)kutumia Helikpota kwenye
chaguzi zake huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni
kujitafutia sifa na umaarufu pekee kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu mkuu wa CCM ambaye pia ni Naibu waziri
wa fedha Mwigulu Nchemba wakati akifungua rasmi kampeni za udiwani
katika kata ya Sombetini .
Mwigulu alisema kuwa CCM inashangaa sana Chadema kutumia Helikpota
kwenye chaguzi nyingi hapa nchini jambo ambalo wanaonesha wazi kuwa
wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya kuongeza sifa kwani gharama
ambazo zinatumika hadi kumalizika kwa kampeni ni zaidi ya Milioni 200.
Alisema kuwa Gharama ambayo inatumika kwenye uendeshaji wa Helkopta ni
gharama ambayo ingeweza kuwasaidia wanachama wao lakini hata matumizi
mbalimbali ya chama hicho ambacho bado kinaonekana kukabiliwa na
changamoto nyingi sana
Chama cha mapinduzi (CCM)kimesema kuwa kinashangazwa na kitendo cha
chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema)kutumia Helikpota kwenye
chaguzi zake huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni
kujitafutia sifa na umaarufu pekee kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu mkuu wa CCM ambaye pia ni Naibu waziri
wa fedha Mwigulu Nchemba wakati akifungua rasmi kampeni za udiwani
katika kata ya Sombetini .
Mwigulu alisema kuwa CCM inashangaa sana Chadema kutumia Helikpota
kwenye chaguzi nyingi hapa nchini jambo ambalo wanaonesha wazi kuwa
wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya kuongeza sifa kwani gharama
ambazo zinatumika hadi kumalizika kwa kampeni ni zaidi ya Milioni 200.
Alisema kuwa Gharama ambayo inatumika kwenye uendeshaji wa Helkopta ni
gharama ambayo ingeweza kuwasaidia wanachama wao lakini hata matumizi
mbalimbali ya chama hicho ambacho bado kinaonekana kukabiliwa na
changamoto nyingi sana
“wananchi wa kata ya Sombetini napendwa kuwaambia kuwa hata sisi
wenyewe huwa tunashangaa sana ujio wa hii Helikopta na ninapenda
kusema wazi helikopta hiyo inakuja ili iweze kuwazubaisha ninyi sasa
msikubali kudanganywa na helikopta baliangalieni sera za mgombea
“aliongeza Mwigulu
Pia aliwataka wananchi kuhakikisha kuwa kamwe hawatumiki kwenye siasa
za sifa na ushahbiki kwani siasa hizo wakati mwingine zinasababisha
hata vifo vya watu ambao hawana hatia ya kufa ovyo
“wananchi mnapswa kujua na kutambua kuwa siasa za sasa zimebadilika
sana msikubali kuwa mashabiki wa siasa bali mnatakiwa kuangalia zaidi
sera za vyama na mahitaji yenu msije mkachagua kiongozi kwa ushabiki
itawagharimu sana kwenye utendaji”aliongeza Mwigulu
Awali Mgombea Udiwani katika kata hiyo ya Sombetini kwa tiketi ya CCM
alisema Bw David Mollel alisema kuwa ana mikakati mingi sana ya
kuhakikisha kuwa anasaidia kata hiyo endapo kama atapata ridhaa ya
kuongoza rasmi kama diwani
David alisema kuwa changamoto ambazo atahakikisha kuwa ameweza
kuzitatua ni pamoja na urekebishaji wa barabara, uboreshaji wa masoko,
kna uimarishaji wa vikundi vya wanawake na jamii kwa ujumla.
DIWANI WA KATA YA KIGERA MUSOMA GABRIEL OCHARO(CUF) APELEKWA RUMANDE.
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Mara imemsomea mashitaka ya kuharibu
mali Diwani wa Kata ya Kigera Gabriel Ocharo(CUF) zenye thamani ya
shilingi milioni 25,300,000 kinyume na kifungu cha 326 ya kanuni ya
adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Imedaiwa
na Mwendesha mashitaka Jonas Kaijage mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi
Mwandamizi Faisal Kahamba Diwani huyo kinyume na kifungu hicho
alishiriki uharibifu wa majengo sita ya madarasa katika shule ya msingi
Kigera A mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ilielezwa
na mwendesha mashitaka kinyume na utaratibu,Diwani huyo alitenda kosa
hilo la uharibifu wa majengo ya madarasa ya shule hiyo na kupelekea
kufanya wanafunzi kushindwa kuhudhuria vipindi madarasani.
Kutokana
na kushindwa kukidhi masharti ya dhamana kulingana na thamani ya
uharibifu uliofanyika katika shule hiyo,Diwani Ocharo alipelekwa rumande
hadi kesi hiyo itakapo tajwa tena februari 2 mwaka huu.
Hivi
karibuni katika kikao cha Baraza la madiwani wa Halimashauri
ya Manispaa ya Musoma lililofanyika chini ya Naibu Meya wa Halimashauri
hiyo Bwire Nyamwero(Chadema) lililotoa agizo kwa Afisa Elimu Msingi wa
Halimashauri hiyo kutoa
taarifa polisi juu ya uharibifu wa majengo sita ya madarasa katika shule
ya
msingi Kigera A uliodaiwa kufanywa na Diwani huyo.
Kwenye kikao hicho, Diwani wa Kata ya Bweri Zidi Sondobhi(Chadema)
alisema katika muhula huu wa masomo wanafunzi wa shule ya msingi Kigera
A wameshindwa kuhudhulia vipindi madarasa kwa kile kilichoonekana
majengo sita ya shule hiyo kung'olewa mabati na kushindwa kuezekwa hali
inayofanya wanafunzi kushindwa kusoma na kuwaaomba madiwani watoe tamko la kumtaka Diwani huyo akamatwe.
Mkurugenzi wa Halimashauri ya
Manispaa ya Musoma Ahmed Sawa alilieleza Baraza hilo hakuwa na barua yoyote wala kutoa maagizo ya
kuondolewa mabati ya shule hiyo hali iliyomfanya Naibu Meya kuomba
maelezo ya kina kutoka kwa Diwani wa Kata husika juu ya uhalibifu
uliofanywa kwenye shule hiyo na baadae kutoa amri ya kufunguliwa mashitaka.
HABARI KWA HISANI YA SHOMARY BINDA.
HABARI KWA HISANI YA SHOMARY BINDA.
HUYU NDO MWANAFUNZI WA KITANZANIA ALIYEUNDA NDEGE YA ABIRIA SHUHUDIA HAPA.
Kijana wa
Kitanzania ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Arusha aitwaye
Denis, amefanikiwa kuunda ndege ya abiria. Kijana huyo alianza kuiunda
ndege hiyo zaidi ya miezi mitatu iliyo pita na sasa ipo katika hatua za
mwisho kabla hajaifanyia majaribio.
Hii ni mara ya pili kwa kijana huyu kuunda ndege baada ya kufanya majaribio mengine huko mkoani Mara ambayo yalikuwa na matunda mazuri. Ndege inayo endelea kutengenezwa na kijana huyu ipo katika eneo la Chuo kikuu cha Arusha kilichopo katika mji mdogo wa Usariver karibu na hifadhi ya wanyama ya Arusha (Arusha National Park).
Hii ni mara ya pili kwa kijana huyu kuunda ndege baada ya kufanya majaribio mengine huko mkoani Mara ambayo yalikuwa na matunda mazuri. Ndege inayo endelea kutengenezwa na kijana huyu ipo katika eneo la Chuo kikuu cha Arusha kilichopo katika mji mdogo wa Usariver karibu na hifadhi ya wanyama ya Arusha (Arusha National Park).
Operesheni Pamoja Daima: Itamtimua huyu bundi Chadema?
Mwaka 2013 ulimalizika vibaya kwa Chadema. Vivyo hivyo mwaka huu
ulianza vibaya baada ya kuingiliwa na ‘bundi’ wa migogoro aliyepania
kukipasua katika makundi mawili.
Hali hiyo iliendana na uamuzi mgumu wa Kamati Kuu
ya chama hicho kuwavua nyadhifa za juu viongozi watatu – Naibu Katibu
Mkuu, Zitto Kabwe, Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na Mwenyekiti
wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Kamati Kuu haikuishia hapo, baadaye ikawavua
uanachama Dk Mkumbo na Mwigamba, huku Zitto akinusurika baada ya
kufungua kesi mahakamani.
Athari za uamuzi huo zilisababisha baadhi ya
viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya Chadema kutofautiana kimsimamo
huku wengine wakifikia hatua ya kujiuzulu nafasi zao.
Miongoni mwa waliojiuzulu ni pamoja na aliyekuwa
Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Said Arfi na wenyeviti kadhaa wa mikoa,
walioeleza wazi kuwa wanapinga Zitto kuvuliwa nyadhifa zake.
Mbaya zaidi ni pale mvutano huo uliposambaa hadi
kwa mashabiki wa kawaida, nao wakaonekana kugawanyika katika makundi
mawili, moja likimuunga mkono Zitto na jingine likibakia upande wa
chama.
Hata hivyo, ingawa agenda hii haikuwekwa wazi,
uongozi wa chama hicho umeibuka na mbinu ya kukabiliana na ‘bundi’ huyo
wa mgawanyiko kwa kampeni maalumu iliyopewa jina la Operesheni Pamoja
Daima, itakayofanyika katika mikoa tisa.
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe anasema
lengo kuu la kuanzisha operesheni hiyo ni pamoja na kukiimarisha chama
na kuwafumbua macho Watanzania juu ya mchakato wa Katiba Mpya
unaoendelea. Operesheni hiyo ya siku 14 inayoendelea katika mikoa yote
isipokuwa Lindi na Mtwara, inaendeshwa na makundi sita ya viongozi
matatu yakitumia helkopta na wengine magari.
Swali la kujiuliza ni je, kufanyika kwa operesheni hii kutasaidia kumfukuza ‘bundi’ huyo aliyeanza kukipasua chama?
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema juhudi
hizo zinaweza kufanikiwa kwa kiwango kizuri kwa kutegemea mwamko wa
kisiasa wa mikoa wanayokwenda.
Ni njia sahihi
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiraia ya kufuatilia
Utendaji wa Bunge (CPW), Marcossy Albanie anakubaliana na uamuzi wa
chama hicho akisema operesheni hiyo ndiyo njia sahihi inayoweza
kukiimarisha zaidi chama hicho. Albanie anasema harakati za kuanzisha
operesheni hiyo ni pamoja na kuongeza mwamko wa Watanzania kabla ya
Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015. Anasema mgogoro uliojitokeza ndani ya
chama hicho hauwezi kuwa sababu pekee ya kuanzisha operesheni hiyo.
NA GAZETI LA MWANAINCHI.
DIAMOND ALIPOFANYA INTERVIEW NA KISS TV NAIROBI KENYA NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI.
Hii ni sehemu ya pili,ya mahojiano na media mbali mbali
Hapa Nairobi,baada ya kufanya mahojiano na
Tuva wa Mambo mseto..nilifanya mahojiano na
Kiss Tv kisha nikafanya na waandishi kutoka vyombo vingine vya habari
waliokuwa wakinisubiri nje...
kama ilivyokuwa kwenye mambo mseto...kikubwa
walitaka kufahamu kuhusu mipango yangu ya baadae
kimziki,collabos,na maisha yangu..
Director wa kipindi,Kiss Tv akiniwekea Mike
Mahojiano na Kiss Tv yakaanza
Waandishi kutoka vyombo vingine vya habari wakinisubiri
Mahojiano yakaanza na wwaandishi wamajarida na magazeti
Subscribe to:
Posts (Atom)