Waziri
wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wa mbele akiwa amesimama juu ya bomba
jipya Boko nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Ulazaji wa bomba hilo
umekamilika kwa asilimia 54. Nyuma yake ni maafisa wa Wizara ya Maji,
Dawasa na wahandisi wa mradi.
Waziri
wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe wa kwanza kulia, akipewa maelezo juu
ya pampu za kusukumia maji. Pampu moja inauwezo wa kusukuma lita milioni
90 kwa siku. Na huwa sinasukuma pampu tatu na moja hubaki akiba endapo
moja itaharibika ili kufanya maji kusukumwa kwa ujazo uliokusudiwa.
Na Athumani Shariff
WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe ametembelea mradi wa ulazaji wa bomba jipya la maji kwenye mradi mkubwa wa maji kutoka Ruvu chini, Mji mdogo wa Bagamoyo, utakao leta maji zaidi ya lita milioni 270 kwa siku.
WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe ametembelea mradi wa ulazaji wa bomba jipya la maji kwenye mradi mkubwa wa maji kutoka Ruvu chini, Mji mdogo wa Bagamoyo, utakao leta maji zaidi ya lita milioni 270 kwa siku.
Mradi
huo uliokamilika kwa zaidi ya asilimia 54 unakabiliwa na changamoto
kubwa mbili zikiwemo za uhaba wa umeme katika kiwanda cha kutengeneza
mabomba jambo ambalo linakwamisha upatikanaji wa mabomba yaliyyokadiriwa
na kampuni hiyo ya Sinohydro inayotekeleza mradi huo.
Changamoto
nyingine iliyoelezwa katika mradi huo ni kesi zilizofunguliwa dhidi ya
Mamlaka ya Maji Safi Dar es Salaam (DAWASA), kesi 12 zipo mahakani
ambazo mamlaka hiyo imepanga kuzishughulikia haraka iwezekanavyo.
Akijibu
swali la waandishi wa habari juu ya hatua zinazochukuliwa na DAWASA
katika kukabiliana na kesi hizo, Mwenyekiti wa bodi ya DAWASA Bi. Hawa
Sinare alisema mpango uliopo ni kuonana na Jaji Mkuu kusaidia kesi hizo
zisikilizwe kwa haraka na zitolewe hukumu mapema ili zisikwamishe mradi
huo mkubwa wenye manufaa kwa watu walio wengi.
Profesa
Maghembe pia alitembelea upanuzi wa mtambo wa kusukuma maji
uliokamilika kwa zaidi ya asilimia 98 wa Ruvu Chini Mji mdogo wa
Bagamoyo uliojengwa ili kuongeza upatikanaji wa maji kwa jiji la Dar es
Salaam, Kibaha na Bagamoyo.
Awali
Mtambo wa maji wa Ruvu chini kabla ya upanuzi ulikuwa ukizalisha lita
za ujazo milioni 180 kwa siku, wakati huu wa sasa utaongeza lita za
ujazo miliono 90 na kufanya lita za ujazo milioni 270 kwa siku kupelekwa
jijini Dar es Salaam.
Kuongezeka
kwa lita hizo za ujazo katika uzalishaji kunatarajiwa kupunguza ukosefu
wa maji kwa wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam na miji ya Kibaha na
Bagamoyo ambao watapata maji kwa matumizi ya majumbani na viwandani.
Waziri
wa Maji pia aliongeza kuwa kazi ya upanuzi pia itaendelea katika mtambo
wa Ruvu juu baada ya kukamilika mradi wa Ruvu chini na tayari pesa zake
zipo zimeshatengwa zaidi ya bilioni 130. Aidha alisema, pia uchimbaji
wa visima na mabwawa utaongeza upatikanaji wa maji na shida ya maji kuwa
historia jijini Dar es Salaam.
Akijibu
swali juu ya kadhia ya maji jijini Dar es Salaam, Profesa Maghembe
alisema, miradi ya maji haihitaji siasa, na wala huwezi ukaijenga kwa
siku moja, nafikiri munaona ujenzi wake, huu mradi ni mkubwa na
unahitaji utaalamu wa hali ya juu na hata kasi yake ya ujenzi munaiona.
“Niwaambie
wakazi wa Dar es Salaam nafahamu tabu wanayoipata kuhusu uhaba wa maji
na kwakulijua hilo ndiyo maana natafuta suluhisho lakudumu, na maji haya
kwa miradi hii yote itakuwa na uwezo wa kulihudumia jiji la Dar es
Salaam mpaka mwaka 2034 bila shida ya maji na pia miundombinu ya
kuongeza upatikanaji wa maji baada ya mwaka 2034 pia ilishawekwa”
aliongeza Waziri Maghembe.
Michuzi blog
No comments:
Post a Comment