SIKU mbili baada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga Dr
Wiliam Mgimwa ambae pia alikuwa ni waziri wa fedha wananchi wa jimbo
hilo wameipongeza serikali kwa kukarabati maeneo korofi ya barabara
ya Masumbo - Kiponzero ili kuwezesha viongozi wa kitaifa akiwemo Rais
kupita bila tatizo.
Zebedayo Kalinga ambae ni mkazi wa
Kiponzero alisema kuwa msiba huo na kama na ule usemi wa kufa
kufahana kutokana na serikali ya mkoa kujaribu kuficha kasoro zote
za miundo mbinu ya kuelekea weneo la msiba jambo ambalo wao kama
wakazi wa jimbo hilo wamefurahishwa na jitihada hizo.
Hata hivyo alisema wangefurahishwa
zaidi iwapo msafara wa Rais Jakaya Kikwete ungepita katika barabara ya
Kalenga - Kiponzero barabara yenye miundo mbinu mibovu zaidi ili
kupitia msiba huo iweze kutengenezwa kama ilivyofanyika katika
barabara ya Masumbo - Kiponzero
Kwani alisema kwa siku nyingi maeneo
ambao yametengenezwa yalikuwa yakisumbua watumiaji wa vyombo vya
usafiri ila kwa kuwa hakuna kiongozi wa kitaifa aliyepata kufika
huku suala hilo lilifumbiwa macho.
Kalinga alisema kwa upande wake mbunge
wao Dr Mgimwa enzi za uhai wake amepigania kweli ujenzi wa barabara na
ubovu wa barabara hiyo ila hakusikilizwa lakini baada ya kifo chake
ndani ya siku mbili barabara imetengenezwa .
Hivyo alisema kama msiba huo mwili
huo ungekaa nchini Afrika kusini kwa mwezi mmoja ama mwaka kulikuwa
kuna uwezekano wa kijiji cha Magunga ambacho toka nchi ipate uhuru
hakijapata maji safi na salama kupatiwa huduma hiyo ili
kuwafurahisha viongozi wa kitaifa .
Kwa upande wake Zuwena Sanga alisema
kuwa ingependeza serikali ya mkoa wa Iringa na Halmashauri ya wilaya
ya Iringa katika kumuenzi mbunge huyo kusaidia kufikisha huduma ya
maji na umeme katika kijiji hicho kama sehemu ya ahsante Dr Mgimwa kwa
utumishi uliotukuka
Pia alishauri viongozi wa ngazi za
chini kuacha kuficha matatizo ya wananchi wakati wa ziara za viongozi
wa kitaifa kwani kwa kufanya hivyo ni kuendelea kuwatesa wananchi wa
pembezeno ambao siku zote maisha yao ni tabu ila viongozi wa juu
wanapowatembelea viongozi wa chini wamekuwa wakificha ukweli halisi wa
maisha yao.
Alisema kutengeneza barabara kwa
ajili ya viongozi wa kitaifa ni sawa na kuwadanganya viongozi hao
ambao walipaswa kuona maisha halisi ya wananchi wao.picha na habari na Fransis Godwin(Iringa) |
No comments:
Post a Comment