Baadaye Burundi walipata penalti baada ya Claude Ndarusanze kuangushwa ndani ya boksi na Ndikumana alipiga mkwaju huo na kupoteza na kufanya mapumziko matokeo kuwa 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, kwenye dakika 61, Christophe Nduwarugira (pichani) aliipigia Burundi bao la kuongoza kabla ya Mauritania kusawazisha dakika tisa baadaye na kufanya matokeo kuwa
2-2.
Wakati wengi wakiamini kwamba mchezo huo utamalizika kwa sare, Ndikumana alifunga moja ya mabao bora kwenye mashindano hayo baada ya shuti lake la umbali wa mita 35 kuzama moja kwa moja upande wa juu kulia wa goli la Mauritania na kufanya filimbi ya mwisho matokeo kuwa 3-2. Chanzo: mwananspoti.
No comments:
Post a Comment