Monday, January 20, 2014

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LATOA TAARIFA KWA WANANCHI, WAZAZI AU WALEZI.


DV7A3218 
WILAYA YA MBARALI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 19.01.2014 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA ITAMBOLEO, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI NA MKOA WA MBEYA, MTOTO LUMIKI S/O RAHIM, MIAKA 06, MMASAI, MWANAFUNZI SHULE YA MSINGI KAPUNGA DARASA LA KWANZA ALIUAWA KWA KUPIGWA NA FIMBO KICHWANI NA MTOTO BEDON S/O SAID, MIAK
A 12, MUWANJI, MWANAFUNZI SHULE YA MSINGI KAPUNGA DARASA LA SITA. CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUDUMISHA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO WANGALI WADOGO ILI WAKUE KATIKA MISINGI NA USTAWI MZURI WA JAMII NA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UHALIFU.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments:

Post a Comment