Daktari mmoja katika mkoa wa
Kaskazini wa Shanxi nchini Uchina amehukumiwa kifo baada ya kupatikana
na hatia ya kuwaiba watoto saba kutoka hospitali aliyokuwa akihudumu na
kuwauza watoto hao kwa wauzaji watoto.
Hukumu hiyo ya kifo hubadilika na kuwa kifungo cha maisha baada ya miaka miwili ya mshitakiwa kubadili tabiaDaktari huyo aliwadanganya wazazi wapya kwamba watoto wao walizaliwa wakiwa na ugonjwa mbaya.Aliwahadaa kwamba iwapo wazazi wangeliwachia serikali jukumu la kuwaangalia basi wangepewa matibabu ya hali ya juu waliohitaji.
Watoto hao wenye afya njema baadaye waliuzwa kwa bei ya maelfu ya madola kwa wauzaji watoto wanaohudumu katika mikoa ilio karibu.
Sita kati ya watoto walioibwa walipatikana na kurudishwa kwa wazazi wao huku mtoto mmoja aliyeuzwa kwa dola 165 pekee akipatikana ameaga dunia kandokando ya barabara ambapo alikuwa amewachwa na muuzaji mmoja wa watoto
No comments:
Post a Comment