Ulinzi ukiimarishwa Baada ya watuhumiwa wa ujambazi kufikishwa mahakamani
Mbele ni mshitakiwa wa nne Mbaruku Hamis akiingia mahakamani
Kutoka kushoto ni mshitakiwa wa pili Elinanzi Eliabu Mshana, Mshtakiwa wa nne Mbaruku Hamis, Mshita
kiwa
wa tatu Juma Mussa ambaye aliyekuwa Askari Magereza kwa Cheo cha Sajini
, Anaefuatia ni Mshtakiwa wa kwanza PC James aliyekuwa Askari Polisi
Wilaya ya Mbeya, na wa mwisho ni Mshitakiwa wa Tano Amri Kihenya .
Wa kwanza kushoto aliye vaa shati la Draft ni Dereva Ezekia Matatila (34) pamoja na wasikilizaji
Moja ya Gari lililotumika kufanya uharifu wa unyang'anyi wa kutumia silaha
Washitakiwa wanne kati ya watano kutoka kushoto juu hadi wa nne wakiwa wanatoka mahakamani chini ya ulinzi mkali.
Mwenye Jaketi la Njano ndiye Mshitakiwa namba moja PC James
Katikati ni Mke wa mshitakiwa wa tatu ambaye ni Askari Magereza Sajini Juma Mussa, Hata hivyo mwanamke huyo alizirai mahakamani wakati mumewe akiwa kizimbani.
**********************************
ASKARI
wawili wa jeshi la Polisi na Magereza pamoja na watu watatu ambao ni raia wa
kawaida wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya wakituhumiwa kwa
ujambazi wa kutumia silaha.
Watuhumiwa
hao watano kwa pamoja walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya
Wilaya ya Mbeya, Michael Mteite wakituhumiwa kwa kosa moja la unyang’anyi wa
kutumia Silaha kinyume cha Sheria kifungu cha 287 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba F8302 wa
Wilaya ya Mbeya ambaye kabla ya kufikishwa mahakamani alivuliwa Uaskari baada
ya kuhukumiwa kijeshi.
Aliwataja
wengine kuwa ni mshtakiwa namba mbili kuwa ni Elinanzi Mshana(22)Mkazi wa Iyela
Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B 500 Sajenti Juma Mussa(37) wa
Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa Iyela na Amri Kihenya(38)
Mkazi wa Iyela.
Akisoma
mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite, Mulisa
alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3, Mwaka huu majira ya saa
11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya Chunya.
Alisema
watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia gari aina ya Pick Up
lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya
ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sreedhar Pasupelet(38)
mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo mawili ambayo ni GX 100 Toyota
Cresta T 782 BEU na Gari linguine ambalo lilikuwa na namba za Chesesi GX
6011832 AINA YA Grand Mark II.
Aliongeza
kuwa mbinu iliyotumika ni watuhumiwa ni watuhumiwa hao kutega magogo barabarani
huku wakiomba msaada kwa madai kuwa magari yao yameharibika na ndipo baada ya
wahanga kusimama waliwapora vitu vyao wakiwa na mapanga ambavyo ni pesa
shilingi Milioni 3.5, Mabegi matatu yenye nguo mbali mbali yenye nguo, Kompyuta
mpakato, simu aina ya Sumsung yenye thamani ya Shilingi Laki mbili pamoja na
simu ya Dereva aina ya Tekno ambayo aliitambua Mahakani na kutumika kama
kielelezo.
Hata
hivyo watuhumiwa wote kwa pamoja walikana kuhusika na matukio hayo ambapo
upande wa Mashtaka ulileta Shahidi mmoja ambaye ni Dereva wa Pick up Ezekia Matatira
ambaye aliwatambua washtakiwa wote watano na kuiambia mahakama kuwa siku hiyo
ya Tukio aliagizwa na Bosi wake kwamba awapeleke wageni Chunya na ndipo
alipotekwa katika eneo hilo huku watekaji wakiagizwa na Maaskari na yeye kufungwa pingu na kutishiwa na panga.
Aidha
kutokana na kesi hiyo Hakimu Mteite aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 15,
mwaka huu ambapo upande wa Mashtaka utaleta mashahidi wengine huku watuhumiwa
wakirudishwa Rumande baada ya dhamana yao kufungwa.
Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu Blog
No comments:
Post a Comment