Wednesday, January 29, 2014

MADAKTARI WOTE WA LIGI KUU TZ BARA WATAKIWA KUWASILISHA VYETI TFF, VPL KUTIMUA VUMBI TANGA, BUKOBA, DAR


images

Madakatri wote wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupitia klabu zao wanatakiwa kuwasilisha vyeti pamoja na wasifu wao (CV) kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufikia Februari 8 mwaka huu.
Wasifu na vyeti hivyo vinatakiwa ili kuwezesha Kamati ya Tiba ya TFF kuandaa mafunzo kwa wataalamu hao wa tiba kwa wachezaji.
Pia TFF itatoa kwa madaktari hao fomu maalumu za vipimo kwa wachezaji ambapo kila mchezaji atatakiwa kufanyiwa vipimo vyote kama ambavyo fomu imeelekeza.
Hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kuendelea kucheza VPL au kuchezea timu za Taifa kama atakuwa hajafanya vipimo hivyo. Machi 1 mwaka huu ndiyo utakuwa mwisho wa kurejesha fomu za vipimo vya wachezaji.
VPL KUTIMUA VUMBI TANGA, BUKOBA, DAR
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Januari 29 mwaka huu) kwa Coastal Union kuikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini.

Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000 na sh. 15,000. Nayo Ruvu Shooting na Mbeya City zitapambana kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kwa viingilio vya sh. 10,000 na sh. 5,000.
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mtibwa Sugar. Viingilio ni sh. 5,000 na sh. 3,000.
Azam itaumana na Rhino Rangers katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Mbagala. Viingilio ni sh. 10,000 na sh. 3,000.

No comments:

Post a Comment