Thursday, January 16, 2014

Meli ya Titanic yaanza kutengenezwa upya kwa Dola za kimarekani 165 milioni nchini China

china-titanic-replica-6d-tragedy-simulator-1-690x494
Na Mwandishi Wetu, 
WENGI wa watu nchini China wanapendelea ujenzi wa majengo makubwa ya kihistoria na magari kadhaa yenye muonekano wa alama ya uchina kama ishara ya kuonyesha ufanisi wao katika uvumbuzi wa vitu mbalimbali duniani.
Lakini basi tena, wachina ni watu katika jamii wanaopenda kufanya mambo makubwa na tofauti na ni wazalishaji wa vitu vingi vya hapa leo duniani, sasa wachina wanatengeneza meli kubwa kwa mfano wa meli maarufu ya Titanic.

Meli ya Titanic iliyozama mwaka 1914 karibu karne moja iliyopita na kuua watu karibu elfu moja, sasa kampuni kutoka uchina ya Star Investment Group katika mkoa wa Sichuan itatumia dola za kimarekani 165 milioni katika kujenga upya meli mfano wa Titanic.
china-titanic-replica-6d-tragedy-simulator-3
Meli hiyo mpya ya wachina itafanana kabisa na meli ya Titanic iliyozama vibaya kwenye kina cha bahari karne moja iliyopita. Meli hiyo itajengwa kwa ushirikiano na kampuni ya serikali ya China Ship building Corporation ya Wuchang inatumika kama sehemu ya hifadhi ya makumbusho katika mkoa wa Sichuan.
Katika meli hii ya replica ni ishara ya uvumbuzi uliotukuka kutoka kwa wachina na watazamiwa kuingiza mamilioni ya fedha kama riba kutokana na alama ya Titanic duniani

No comments:

Post a Comment