Hata wale wakala wa magodoro na huduma nyingine zote wamejumuika kwenye mgomo huo. |
Hakuna huduma kabisa mitaa hii ambayo hukusanyisha wanunuzi wa mahitaji ya bidhaa mbalimbali.. |
Na maduka ya huduma kwa bidhaa za kielektoniki pamoja na vifaa vya kuendesha mashine na injini imesitishwa kupitia mgomo. |
Wafanya biashara wa vyombo vya elektoniki nao waunga mkono mgomo huo. |
Umekuwa kama mji wa kale uliokimbiwa. |
Kweupeeeeee. |
HALI ILIVYO KATIKA ENEO LA TANGANYIKA. |
Wafanyabiashara
wamekutana hapa katika kituo cha zamani cha mabasi cha Tanganyika
wakiwa na mabango yao yanayowasilisha ujumbe wa kukinzana na ujio wa
mashine hizo ambapo mbali na makato yake pia kodi nyingine hutozwa
pembeni hali wanayoitafsiri kama unyonyaji.
Jijini
Mwanza hususani eneo la katikati ya jiji barabara ya Nyerere, Kenyata,
Lumumba, Libert na maeneo yote ya wilaya ya Nyamagana leo wafanyabishara
wake katika maeneo hayo waliingia katika mgomo wa kutofungua maduka yao
kupingamashine za kutolea risiti za elektroniki (EfDs) ambazo zipo katika mfumo wa uhakiki wa ukusanyaji kodi.
Wafanyabishara
hao wamelalamika kuwa mbali na kuwepo kwa mashine hizo za EfDs zinazo
hakiki mauzo yao na utozaji kodi lakini pia wamekuwa wakiongezewa kodi
kila kukicha.
Wamesema
kuwa matatizo ya mashine hizo ya kuharibika mara kwa mara, kushindwa
kutoa mahesabu ya siku kwa wakati na kushindwa kuprint risiti ni kero
kwao.
. PICHA ZOTE na Sammy Poneka.
Hali si
nzuri sana jijini Mwanza kutokana na mgomo wa wafanyabiashara
wa jiji la mwanza ulionza leo asubuhi....Kwa mujibu wa paparazi
wetu aliyeko jijini Mwanza muda huu, maduka yote yamefungwa na
wafanyabiashara hao wako barabarani muda huu na mabango yao
wakielekea viwanja vya Tanganyika....
Chanzo cha mgomo huo kinadaiwa kuwa ni mashine za TRA ambazo zimekuwa zikipingwa kila kona ya nchi..
No comments:
Post a Comment