Meli ikishusha mizigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam, Mamlaka ya
Bandari Tanzania na wadau wake kuanzia sasa wataanza kufanya kazi saa 24
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na wadau wake, kuanzia sasa
wataanza kufanya kazi kila siku kwa mwaka mzima ili kuongeza ufanisi
ikiwa ni utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban
Mwinjaka alisema hayo jana wakati wa utiaji saini makubaliano kati ya
wizara hiyo, TPA na wadau mbalimbali.
Mwanjika alisema lengo la mkataba huo ni
kuhakikisha TPA kwa kushirikiana na wadau wote, wanafanya kazi kwa saa
24, siku saba za wiki kwa mwaka bila kupumzika.
Miongoni mwa wadau 15 waliotiliana saini ni
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Chama cha Wakala wa Forodha na
Uondoshaji Shehena Tanzania (Taffa), Benki za NMB, CRDB na Chama cha
Wenye Magari ya Mizigo (Tatoa).
Kabla ya mpango huo, bandari imekuwa ikifanya kazi
kwa saa 24 kwenye maeneo muhimu, lakini wadau wamekuwa wakifanya kazi
kwa muda wanaojipangia wenyewe hivyo kukwamisha baadhi ya kazi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Madeni Kipande
alisema kila mdau atatakiwa kutekeleza wajibu wake kama mkakati wa
kufikia malengo ya mpango huo.
“Hivyo mdau yeyote asipotekeleza yaliyo kwenye mkataba, atakuwa amekwamisha mkakati mzima,” alisema Kipande.
wa kuboresha shughuli za bandari zetu,” alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wadau hao, Mwenyekiti wa
Taffa, Steven Ngatunga alisema wizara hiyo itatakiwa kuwachukulia hatua
wadau wasitekeleza wajibu wao.
“ Mizigo inapocheleweshwa kutolewa bandarini kuna
wanaofaidi na kuna wanaoumia, hii ina maana wenye mizigo wanatozwa faini
lakini kuna wadau wanaosababisha hilo hawatozwi faini, sasa hivi yoyote
atakayechelewesha mizigo apewe adhabu,” alisema.
Ngatunga ambaye alitishia kutosaini mkataba huo
kutokana na mapungufu yaliyopo, baadaye alisaini baada ya Katibu Mkuu
kumweleza kuwa kila wakati kutakuwa na mabadiliko yenye lengo la
kuboresha mpango huo.
Aliipongeza Serikali kuwa kuanzisha mpango huo wenye lengo ya kuboresha ufanisi katika bandari hiyo.
“Napongeza kuanza kwa utekelezaji wa mpango huu licha ya
kuchelewa kuanza kwa sababu nilishatoa ushauri miaka mingi iliyopita,”
alisema.
Wadau wengi waliotia saini ni Mkemia wa Serikali,
wizara ya Ujenzi, Wizara ya Kilimo na Chakula, Wizara ya Uvuvi na
Mifugo, Wakala wa Vipimo na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
Wengine ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena Bandarini (Ticts).
Chanzo;Mwananchi.
Chanzo;Mwananchi.
No comments:
Post a Comment