Na Maimuna Kubegeya, Mwananchi
Kwa ufupi
Ni mbinu ya wauzaji kuongeza idadi ya watumiaji,inasemekana huwekwa kwenye vyakula vya watoto.
Dar
es Salaam. Tahadhari imetolewa kwa wazazi kuwa makini na vyakula
wanavyokula watoto wao kufuatia kuibuka kwa mbinu mpya ya wauzaji dawa
za kulevya kuweka dawa zao hizo kwenye vyakula vinavyopendwa na watoto.
Akihutubia
kwenye mkutano wa Baraza la Vijana wa Wilaya ya Temeke, Mbunge wa Jimbo
la Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile amesema, wauzaji wa dawa za kulevya
kila siku wamekuwa wakibuni njia mpya za kuhakikisha wanapata kundi
kubwa la watumiaji wa dawa hizo.
Katika
kuhakikisha dhamira yao hiyo inatimia, hivi sasa wamebuni njia mpya ya
kuweka dawa hizo kwenye vyakula vidogo vidogo vinavyopendwa na watoto
kama vile kashata na ubuyu.
“Ni
jukumu letu sote pamoja na nyinyi vijana ni kuelekeza nguvu zetu katika
mapambano ya dawa za kulevya kwani, kwa sasa yanaonekana kuwa janga la
kitaifa kutokana na kuathiri nguvu kazi kubwa ya taifa letu,” alisema.
Amesema
takwimu za kitaifa za matumizi ya dawa za kulevya kwa Wilaya ya Temeke
siyo nzuri kwani zinasikitisha mno, kwani mmoja kati ya wanawake watatu
wanaotumia dawa hizo ameathirika na Ukimwi huku wa wanaume wawili kati
ya wanne wameathirika na Ukimwi.
Kuhusu magonjwa mengine, amesema kama yale ya homa ya ini pia ni hatari kwa afya na huwaandama vijana hao.
Naye
Mwenyekiti wa Vijana wa Wilaya ya Temeke, Oliver Mwambope amesema,
kutokana na ukweli kuwa vijana hujiingiza kwenye wimbi la matumizi ya
dawa za kulevya, chama chake kimeweka utaratibu maalumu wa kupambana na
tabia zote hatarishi zikiwamo zile za matumizi ya dawa hizo.
Mara kwa mara tumekuwa tukiendesha kampeni za kupambana dawa za kulevya pamoja na tabia nyingine hatarishi.
Pamoja
na utaratibu huo, Mwampombe alisema, hutumia hadhira hususani
zinazowahusu vijana kukumbushana kuhusiana na mapambano hayo.
Baraza
la Vijana wa Temeke, hufanyika kila mwaka mara moja likiwajumuisha
wajumbe wa umoja wa vijana wa vijana kutoka katika kata zote za majimbo
ya Temeke na Kigamboni wakilenga kujadiliana masuala mbalimbali
yanayohusu mustakabali wa maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment