Thursday, February 6, 2014

FAMILIA KUMI NA TANO HAZINA MAHALA PAKUISHI GEREZA PAWAGA

 Ofisi za Gereza Pawaga zilizo ezuliwa na upepo mkali ulio ambatana na mvua juzi jioni.
 Sehemu ya masalia ya bati na matandiko yalio haribiwa na mvua
 SACAP Deusdedit Kamugisha Afisa wa Magereza Mkoa wa Iringa pichani kulia akiongozana na Mkuu wa gereza Pawaga SP.Sosthenes Mwakapala akikagua uharibifu ulio jitokeza katika nyumba za askari na majengo wanayo tarajia kuhamia kwamuda.

 Bustani ikiwa imeharibiwa na Mvua ilionyesha ikiwa na upepo mkari 
Baadhi ya Vyombo vya familia za Askari Magereza vikiwa nje baada ya Mvua kuharibu makazi yao.
Nyumba kumi na tano za Askari Magereza wa Gereza Pawaga wilaya ya Iringa zimeezuliwa na Upepo mkali ulio ambatana na mvua kubwa ya mawe ilionyesha juzi majira ya saa 9 alasiri mpaka saa kumi na moja jioni na kuanza tena saa mbili ya usiku mpaka saa tano usiku.
Akiongea na mwandishi wa habari Mkuu wa Gereza la Pawaga SP.Sosthenes Mwakapala alisema adha hiyo ya mvua imesababisha familia hizo kukosa mahala pa kuishi pamoja na thamani zilizo salia wakati walipokumbwa na mvua hiyo ingawa hakuna madhara kwa binadamu sambamba na hilo kumeezuliwa ofisi za tano za gereza zinazojumuisha Stoo, Bohari, Mapokezi, Utawara pia Bafu ya wafungwa.
 Madhara mengine yaliyo jitokeza ni kuharibiwa vibaya kwa heka tano za Bustani ya gereza yenye mazao mchanganyiko ikiwamo mashina ya Ndizi, Mipapai, Mihogo, Mahindi pamoja na Miwa mimea hiyo imevunjika kabisa haitegemewi  kupona tena.
Mkuu wagareza la Pawaga SP. Sosthenes Mwakapala alisema wao kama uongozi wagereza na viongozi wasaidizi wake wamechukua jukumu la kuhakikisha askari hao na familia zao wanapata mahali pakujihifadhi kwa muda wakati wakisubiri ufumbuzi toka ofisi ya Magereza mkoa wa Iringa. Kwakuwahamishia katika majengo ya Shule ya Msingi, Bwalo la gereza, Ghala la chakula  wakae kwa muda.na mjengwa blog

No comments:

Post a Comment