Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman
Tanzania
Jumatatu imeadhimisha siku ya sheria nchini humo huku changamoto kubwa
ikiwa ni utoaji haki kwa wakati kutokana na matatizo yaliyopo kwenye
mfumo wa mahakama nchini humo.
Kucheleweshwa
kwa kesi bila sababu za msingi kunaochangia mlundikano wa mahabusu
magerezani umekuwa chanzo cha malalamiko kutoka kwa wananchi na wadau
mbali mbali wa sheria nchini Tanzania hali inayochangia vyombo hivyo vya
kutoa haki kulalamikiwa.
Rais Jakaya
Kikwete aliyeshiriki maadhimisho hayo ya siku ya sheria nchini humo pia
alisisitiza suala hilo la utoaji haki kwa wakati huku akitumia fursa
hiyo kusisitiza kwamba serikali itaendelea kuziwezesha mahakama nchini
kwa kuziongezea bajeti, kupanua wigo wa ujenzi wa mahakama za mwanzo na
wilaya na kuboresha majengo ya mahakama zilizopo pamoja na kuongeza
rasilimali watu katika kuhakikisha vyombo hivyo vya kutoa haki
vinatimiza wajibu wao kwa ukamilifu.
kwa
upande wake Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman amesema pamoja
na changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya mahakama nchini, zikiwemo
upungufu wa mahakimu na vitendea kazi, mahakama itaendelea kuboresha
utaoji wa huduma baada ya kuanzisha mpango maalum ambapo kesi zote za
jinai na madai zinatakiwa kumalizika katika kipindi cha miaka miwili
kuanzia sasa
Kauli mbiu ya siku ya sheria nchini Tanzania ni utendaji wa haki kwa wakati umuhimu wa kuwashirikisha wadau.
CHANZO:VOA
No comments:
Post a Comment