Tuesday, February 11, 2014

TAARIFA TOKA CHADEMA Kuhusu matokeo ya uchaguzi mdogo wa Udiwani 09/02/ 2014




Kuna mambo mengi yamezungumzwa tangu jana na hadi leo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa marudio katika kata 27 na ushindi wa CHADEMA katika kata 3 za Kiborloni, Sombetini na Njombe mjini.

Tutaendelea kusoma, kusikiliza na kupokea kila aina ya criticism, zinazotolewa kwa njia mbalimbali, ingawa hatimaye tutafanyia kazi constructive criticism zinazojengwa katika dhamira ya kweli na nia njema kwa ajili ya mustakabali wa Watanzania na chama chao, CHADEMA.

Moja ya masuala yanayozungumzwa na wapinzani wa CHADEMA, ambayo hata leo katika press conference iliyoitishwa Lumumba, litazungumza sana, ni kujaribu 'kuoanisha' M4C-OPD (matumizi ya chopa 3) na ushindi wa kata 3.

Kuoanisha mambo hayo kwa mgongo wa kufanya uchambuzi au tathmini ya mambo hayo mawili, ni ama kuamua kuwa myopic kwenye hoja muhimu au kuamua kupotosha kwa makusudi ya propaganda nyepesi au kutokujua tu.

Wakati Mwenyekiti Mbowe anazindua M4C- Operesehni Pamoja Daima, mbele ya waandishi wa habari alisema malengo ya shughuli hiyo maalum kuwa itaweka msisitizo au mkazo kwenye masuala makuu yafuatayo;

  • Mchakato wa katiba mpya Daftari la wapiga kura Wazawa na rasilimali za nchi yao Ugumu wa maisha unaosababishwa na uongozi mbovu na sera zilizoshindwa za CCM

Kwa wale waliofuatilia OPD, kila mtu anajua namna ambavyo imeibua mjadala mkali katika masuala hayo, kuanzia na katiba mpya, wazawa na matumizi (unufaikaji) ya rasilimali, ugumu...

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikalazimika kutangaza kwamba tayari serikali imetoa fedha za kuboresha daftari la wapiga kura. Haitoshi tu kusema hivyo. Viongozi wakuu, Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Dkt. Slaa wakatoa kauli ya chama wakiitaka NEC itoe taarifa kamili juu ya mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na;
  • Ratiba kamili ya shughuli hiyo Lini NEC itaanza kukagua vituo Tarehe rasmi ya kuanza kuboreshwa daftari Serikali imetoa bajeti ya kiasi gani (inatosha kwa shughuli nyeti kama hiyo?

Kwa sababu M4C-OPD ilikuwa ni ya nchi nzima, yako maeneo ya uchaguzi ambako chopa zilifika. Lakini kuoanisha matumizi ya chopper 3 na matokeo ya ushindi wa kata 3, ni kulazimisha hoja isiyokuwepo kwa premises za kuokoteza Wapinzani wa CHADEMA wakisukumwa na euphoria ya ushindi usiokuwa na uhalali (tutafafanua), wamejikita kwenye 'negative (ya picha)' inayozungumzia chopper 3 kwa kata 3, wanashindwa kuiona 'picha kubwa' (negative Vs bigger picture), inayozungumzia masuala kadhaa, mfano;

Katika uchaguzi wa 2010 matokeo yalikuwaje?
Je kuna mabadiliko ya goal post, figures na namba?
Je mabadiliko hayo yako in favour of status quo au yanasapoti vuguvugu la mabadiliko?
CHADEMA itajikita katika hayo kwa sababu ni muhimu sana katika suala kulinda demokrasia ya watu na kusheherekea ushindi, hasa ushindi ulio halali.

Mfano; katika Kata ya Njombe mjini, mwaka 2010 CHADEMA haikusimamisha mgombea kabisa wa udiwani wala ubunge. Mgombea Urais wa CHADEMA alimzidi kwa mbali mno mgombea urais wa CCM. Mbali mno.

Matokeo ya jana katika kata hiyo hiyo kwa uchaguzi wa udiwani, yanaonesha kwamba;

CHADEMA imepata kura 2,202 CCM imepata kura 1,094
Jumla ya kura zilikuwa 3334
Jumla ya vituo vilikuwa 41, CCM imeshinda kituo kimoja tu kwa tofauti ya kura 9

Iko mifano mingi ya namna hii katika uchaguzi wa jana. Kuna maeneo ambayo CHADEMA haikuwahi kuweka mgombea, imetoa ushindani mkali na kuna maeneo ambayo uchaguzi uliopita kulikuwa na tofauti kubwa mno ya kura, lakini safari hii gap limepunguzwa kwa namba kubwa sana. 

Mfano Kata ya Mpwayungu, Mtera, Dodoma Mwaka 2010
CHADEMA 602
CCM       1812 
Mwaka 2014 (jana)
CHADEMA 555
CCM         872

Katika Kata ya Ubagwe, mwaka 2010, CCM ilipita bila kupingwa. Uchaguzi wa jana umekuwa;

CCM 329
CHADEMA 215
TADEA 71
Zilizoharibika 3
Where are the voters? Where is legitimacy? 
Moja ya masuala ya msingi sana ambayo tulitarajia yawaumize kichwa sana watu, hususan walioko madarakani ni swali hili; Je wapiga kura wako wapi?
Suala hili limepewa uzito na CHADEMA pamoja na wapenda demokrasia na maendeleo wengine wengi tu nchini tangu baada tu ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Nani anajali?
Walioko madarakani wangelikuwa wanathamini mchakato wa demokrasia ya uwakilishi, ambayo maana yake ni kuwaheshimu watu/wapiga kura, kamwe wasingekuwa wanakimbilia kushangilia matokeo, tena yasiyowapatia uhalali.
Mathalani
Kata ya Ubagwe, Ushetu, Shinyanga
Wapiga kura walioandikishwa wako 4270
Waliopiga kura jana ni 618
CCM wameshinda kwa kura 329 dhidi ya CHADEMA kura 215, TADEA- 7, zilizoharibika 3. 
Kata ya Nyasura Bunda, 
Waliojiandikisha ni 5333
Waliopiga kura      1579
Wapiga kura wako wapi? Uko wapi uhalali wa ushindi wa kata nyingi?Aidha, wapinzani wa CHADEMA hawataki kabisa kabisa kuzungumzia irregularities. Very serious irregularities done purposefully. Hawataki kabisa kugusia namna ambavyo watu wamepigwa wazi wazi na kuchukuliwa kwenye vituo vya kura, wakiwemo mawakala wa CHADEMA kisha eti wakapelekwa vituo vya polisi.
Wapenda demokrasia hao ya ushindi, hawataki kabisa kuzungumzia mapanga na mashoka yaliyotembezwa jana na Green Guards! 
Huwezi kuzungumzia kushindwa au kushinda kwenye matokeo ya jana au mengine yoyote yale, bila kujadili masuala hayo kwa upana sana, unless kama tumekubaliana kuwa iwe ni sehemu ya demokrasia yetu, watu kukatwa mapanga, mashoka, damu kumwagika, watu kukamatwa vituoni bila makosa, kisha CCM wakaachwa wanafanya wanavyotaka, wakuu wa wilaya kuingia vituoni na kutoa maagizo.
Labda kwao ni sehemu ya mchakato wa kuchagua wawakilishi! Vinginevyo basi tuanze kuwaandaa Watanzania kwa uchafu wa namna hii.
Kwa kusema haya kamwe haimaanishi kuwa CHADEMA haihitaji kufanya tathmini ya kitaalamu, kitaaluma na kina sana. Itafanyika na itakuwa muhimu kwa ajili ya kuendelea kujiimarisha na kujipanga katika mapambano haya. 
Lakini kwa vyovyote ni muhimu sana sana, kuweka mikakati ya kukabiliana na Intarahamwe inayotaka kupandikizwa Tanzania na Watawala dhidi ya Watanzania.
Suala hili la Green Guards kufanya maovu dhidi ya wapinzani wa CCM kwenye uchaguzi, tena mahali pengine uovu wa kutisha unaohusisha silaha, kwa namna ile ile ya Intarahamwe, mbele ya askari polisi, wala wasiguswe, wapo wengine bado wanaliona kuwa ni jambo dogo au mzaha fulani hivi.
Siku madhara yake yatakapokuwa yameshafika mfupani, tutajua Intarahamwe ilikuwa ni kitu gani, kilianzaje, kilipataje nguvu na matokeo yake yalikuwa ni nini. 
Where are the voters, where is legitimacy?

Tumaini Makene
Afisa Habari-Chadema.

No comments:

Post a Comment