Monday, February 10, 2014

WAZIRI MAGHEMBE AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA MFUKO WA WANYAMAPORI DUNIANI

OLYMPUS DIGITAL CAMERAMkurugenzi wa WWF- Tanzania Bw. Bell’Aube Houinato akizungumza na waziri wa maji, Profesa Jumanne MaghembeOLYMPUS DIGITAL CAMERAWaziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe akieleza  jambo kwa wageni wake
.
Na Rehema A. Omari
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe leo amekutana na Mkurugenzi mkazi wa Mfuko wa Wanyamapori Duniani (WWF) Bell’Aube Houinato leo makao makuu ya Wizara ya Maji, Ubungo jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Maji.
Bw. Bell’Aube alimuelezea Waziri wa Maji kwa ufupi kazi ambazo WWF inazifanya Tanzania na namna ambavyo Sekta ya Maji inahusika katika shughuli za utunzaji wa mazingira pamoja na viumbe hai.
Pia alichukua fursa hiyo kumshukuru Profesa Maghembe pamoja na Serikali kwa ushirikiano wanaotoa kwa shirika hilo. “ napenda kuishukuru Wizara yako pamoja na serikali kwa ujumla kwa ushirikiano ambao mmelipatia shirika la WWF” alisema Bell’Aube
Mratibu wa Programu za Maji, Kelvin Robert ambae aliambatana na Mkurungezi huyo, alieleza kwamba WWF -Tanzania kwa sasa ina programu tano zinazohusu Viumbe aina, Bahari, Maji, Misitu na Mashirika ya Kiraia. Ambapo katika programu ya maji, WWF imekua ikifanya kazi na Mabonde ya Maji ya Rufiji, Ziwa Victoria, Wami Ruvu na bonde la Pangani ambapo kazi yao kubwa ni kushirikiana na Ofisi za Bonde katika kuunda vyama vya watumiaji maji, kujenga uwezo katika Usimamizi wa Rasilimali za Maji, elimu ya mazingira na  uhifadhi wa vyanzo vya maji na  kuwawezesha wananchi kufanya shughuli mbadala.
Baada ya kupata taarifa hiyo fupi Profesa Maghembe alishauri zitafutwe mbinu za namna gani wananchi wanafaidika na programu ya maji ya shirika hilo “ni kitu gani mnawafanyia wananchi ili wawezekufaidika na shughuli zenu, kama mnatunza mazingira wananchi wanafaidika vipi na utunzaji huo. Inabidi mtafute njia ambazo mnaweza kuwasaidia wananchi kupata maji pamoja na kwamba shughuli zenu ni za kimazingira. Alisema Waziri Maghembe.
Profesa Maghembe pia alisisitiza kwamba ni muhimu shirika hilo lifanye kazi kwa karibu na Idara ya Rasilimali za Maji ili waweze kuona ni namna gani wanaweza kufikia lengo la kuwapatia wananchi maji.
Aidha Bw. Bell’Aube alimueleza Profesa Maghembe kwamba katika mpango kazi wao wa miaka mitano ijayo swala la Usimamizi wa Rasilimali za maji ni moja kati ya vitu muhimu ambavyo wanataka kuvifanyia kazi kwa karibu wakishirikiana na wadau wengine ambao wanaweza wakasaidia katika kusaidia katika Sekta ya Maji

No comments:

Post a Comment