Namna mdomo unavyoharibika kutokana na ngono kufanywa kwa kutumia mdomo.
Leo
ni siku ya Saratani Duniani. Wakati tunaadhimisha siku hii hapa nchini
idadi ya vijana ambao ni tegemeo la taifa inazidi kupungua kutokana
kuangamia kwa saratani ikiwemo ya koo.Utafiti
uliofanywa na Shirika la Afya Dunani (WHO) nchini umeonyesha asilimia
20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral
Sex”.Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili,pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.Utafiti
unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi
vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai
wao.Katika utafiti huo wa hivi
karibuni, ulibaini wanaume 747 na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila
mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni
wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti
unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20
hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo
likiwa ni kuwavutia wapenzi wao katika kushiriki ngono.
Vijana
wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo
kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake.
Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya
vitendo hivyo.
Utafiti
unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo
wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na
saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road,
Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya koo ni ya pili katika mtiririko
wa saratani zinazowapata wanaume nchini, ikiongozwa na ile ya ngozi
(Karposi’s Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna
saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.
Anasema
mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani ya koo
kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na umri mkubwa ambao
huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya
ngono ya mgomo.
“Hali hii
ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na ujana,
wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani
tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze kumvutia mwanamke anamfanyia
hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa,”
anasema Dk Kahesa na kuongeza.
“Kuna
njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara
yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na
mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo
wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama
wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,”anaongeza
Sababu nyingine zaidi
Anasema
staili ya maisha nayo imechangia kuongezeka kwa ugonjwa huo, vijana
wengi kwa sasa hutumia muda mwingi kuangalia video za ngono na staili
zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi ya ngono
ya mdomo.
Dk Kahesa
anasema asilimia 12 ya wagonjwa wote wa saratani nchini wanasumbuliwa
na saratani ya koo, hivyo kuna kila sababu kwa vijana kubadilisha tabia
na kuepuka kuiga mitindo ya wenzetu wazungu ambayo mara nyingi
inapotosha mila na tamaduni za Kiafrika.
Anasema
katika mtiririko wa saratani zinazoongoza nchini saratani ya koo
inashika nafasi ya tano, wagonjwa wengi wanaopatwa na ugonjwa huo ni
watu wenye umri mkubwa wa miaka 60 na kuendelea hiyo inaonyesha kuwa
wengi wao walianza ngono ya mdomo muda mrefu wakati wakiwa bado
wadogo.
“Asilimia
kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo nchini, inawapata watu
wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kutokana na wengi wao
kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati bado wadogo au
wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao,” anasema Dk Kahesa.
Aina ya kansa ya koo
Tafiti
zinaonyesha kuna aina mbili za saratani ya koo; aina ya kwanza ni
“Oesophagus Carcinoma na Squamous cell carcinoma, zote hutofautiana
wakati zinapimwa kwenye darubini lakini matibabu yake yanafanana.
Aina hizo
ndizo zilizopo nchini na huanza mapema kuharibu seli ambazo zipo
katika utandu uliopo katika ukuta wa koo kabla ya kuenea katika maeneo
mengine ya koo.
Visababishi vya kansa ya koo:
Moja kati
ya vitu vinavyosababisha kansa ya koo ni mwenendo wa maisha yetu kwa
kula vyakula vyenye asidi, vyakula vichachu, vyakula vyenye pilipili,
pombe kali na vyakula vigumu ambavyo hukwaruza koo na hivyo kusababisha
saratani.
Anasema
asilimia 90 ya wagonjwa wanaopokelewa katika Taasisi ya Saratani ya
Ocean road wanakuwa na historia ya kutumia vikali kama pombe kali,
kuvuta sigara kwa kupindukia, kula pilipili kwa wingi na kutumia vitu
vyenye uchachu.
Dalili za saratani ya koo
Moja kati
ya dalili za mgonjwa wa saratani ni chakula kukwama kwenye koo, siku
za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha
majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate.
Ugonjwa
huo unachukua muda mrefu kugundua na kuona viashiria kwani mwanzo
mgonjwa huanza kupata shida kumeza chakula na kwamba wagonjwa wengi
wanaofika katika Taasisi hiyo ya Saratani wanakuwa tayari wamechelewa
kwani wanakuwa katika hatua ya mwisho.
“Unaweza
usionyeshe dalili lakini kadri siku zinavyokwenda ndiyo kunakuwa na
dalili zinajitokeza pia katika kipindi hicho mtu anakuwa na maumivu
wakati wa kumeza chakula, maumivu katika kifua na mgongo na hata
kupungua uzito pamoja na kikohozi kikavu kinachoweza kudumu mwezi
mmoja,” anasema.
Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Kwanza
mtu mwenye ugonjwa huo anapaswa kuhawi hospitali ili aanze matibabu
mapema kutokana na ukweli kwamba mgonjwa anayewahi kupata matibabu ana
uwezekano wa kupona kuliko yule ambaye amechelewa kugundulika na kuanza
matibabu.
Kama
saratani hiyo itakuwa imeshambulia viungo vyote vilivyopo jirani na
koo na hadi kufika katika tezi au kiungo kingine cha mwili, mgonjwa
anaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji, kutumia mionzi na hata kifaa
maalumu ambacho ni kemikali.
Tafiti zilizofanywa nchini
Wataalamu
mbalimbali nchi wamefanya tafiti zinazohusiana na ugonjwa huo na kusema
kuwa kati ya mwaka 1983 hadi 1992 kulikuwa na kati ya watu 546
waliopimwa, wanaume 430 na wanawake 116 waligundulika kuwa na ugonjwa
huo.
Utafiti
huo ulishirikisha watu wenye umri wa miaka 21 hadi 90, ulibaini kuwa
wagonjwa wengi walikuwa wenye umri wa miaka 50-59 tofauti na hali
iliyopo sasa ugonjwa wa kansa ya koo unawaathiri vijana wenye umri wa
miaka 40.
Dk Kahesa
anasema katika kipindi cha miaka saba iliyopita takwimu za taasisi yake
imeongezeka kutoka kutoka wagonjwa 167 hadi kufikia wagojwa 277. Hali
inaonekana huenda ikaongezeka kutokana na ukweli kwamba wengi wa watu
wanaonekana kuendeleza tabia hatarishi zikiwemo hizo za kutumia midomo.
Magonjwa mengine sehemu za siri
Miongoni
mwa magojwa ambayo yanaweza kumpata mtu ambaye ananyonya au kulambana
sehemu hizo ni pamoja na gonjwa wa gonoreha, ambapo ugonjwa huu huanzia
katika koo na mwanzoni huhisi kama ni ukavu wa kifua au maradhi ya
kawaida ya kifua, ila baadaye hushuka na kuelekea katika viungo vya
uzazi.
Ugonjwa
mwingine ni kaswende ambao huambukizwa kirahisi zaidi kupitia mdomo na
hasa pale inapotekoa mdomo unapokutana na kiungo chenye athari hizo.
Vile vile
ugonjwa wa chlamydia ni moja wapo kati ya magonjwa ya zinaa ambao
huambukizwa kwa bakteria na kwamba ugonjwa huu pia huambukizwa kupitia
mdomo, ingawa waathirika wanaweza wasijijue maana huwa hauna dalili kwa
muda mrefu.
Hepatitis
A: Hiki ni ni kirusi kinachopatikana katika kinyesi cha binadamu,
kirusi hiki huwaingia wale wanaopenda kunyonya na kulambana sehemu za
haja kubwa. Ni kwamba kwa ugonjwa huu mtu anaweza akaharibika macho hadi
kupofuka.
Hepatitis
B: Ugonjwa huu huambukizwa kama virusi vya Ukimwi kwa sababu virusi
vyake hukaa katika majimaji yanayotoka katika sehemu za siri na damu.
Mtu akiwa na ugonjwa huu, mwili wake unakuwa na vipele vingi na hata
majipu ambayo huwa magumu kupona na wapo wanaokufa.
Vile vile
ugonjwa wa Hepatitis C: ni ugonjwa ambao hupatikana pindi damu
inapotoka maana vijidudu vyake vinakaa katika damu. Ugonjwa huu humfanya
mtu kuvimba viungo na hata kukatika.
Hata
hivyo kupitia staili hii yaupeana raha kwa kunyonyana sehemu za siri,
kuna uwezekano wa kupata maambukiz ya virusi vya Ukimwi kwa uchache
lakini kwa nchi zilizoendelea wamebuni aina ya kondom ambazo huvaliwa
katika mdomo wa binadamu na hivyo kupunguza hatari ya kupata madhara
hayo.
JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
Dk Kahesa
anasema hakuna utafiti wa moja kwa moja unao onyesha kuwa baadhi ya
wanaume wanaofanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na upungufu wa nguvu
za kiume.
“Utafiti
wa mtu mmoja hautoshi kuonyesha kuwa baadhi ya wanaume wanafanya ngono
kwa njia ya mdomo wanakuwa na ukosefu wa nguvu za kiume, hivyo
kinachotakiwa ni kufanya utafiti wa kina ili kubaini kama tatizo hilo
lipo licha ya kuwepo kwa kesi nyingi zinazodaiwa kuwa baadhi ya wanaume
hawana nguvu za kiume na wapenzi wao huwafichia siri kwa kufanya nao
mapenzi kwa njia yam domo”anasema.
NINI KIFANYIKE:
Wataalamu
wa masuala ya ndoa na saikolojia wanasema kuna njia nyingi za kuandaana
wakati wa tendo la ndoa tofauti na kunyonyanyana sehemu za siri.
Wataalamu
hao wanasema sio sahihi kwa mwanaume au mwanamke kunyonyana sehemu za
ndoa mwenzake na kwamba staili hizo ni staili za wanzetu wa nje lakini
kitu kinachosababisha kukua kwa kasi kwa staili hiyo ya kunyonyonyana
sehemu za siri au kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni kutokana na kasi
ya utandawazi.
Wadadisi
wa mambo wanadai kuwa baadhi ya watu huiga staili hizo kutoka katika
mitandao bila kujali kuwa kuna zina madhara makubwa, hivyo ni jukumu la
kila mtu kulinda afya yake na ya mwenza wake.
Sio kila kitu kinachowekwa katika mitandao ya kijamii kina manufaa la hashaa! vitu vingine vinachangia kuhatarisha maisha.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment