Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu
wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga
ni biashara
na kilimo.
Wachagga ni kabila la tatu kwa
ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya
Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000.
Vikundi
vya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya
asili yao na maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la kichagga ni
mkusanyiko wa makabila madogo madogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia
kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia Mashariki Tarakea, Rombo hadi magharibi ya
Kilimanjaro Siha, Machame.
Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Marangu,Wa-Kilema, Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame. Makundi
mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vunjo, Wa-Uru, na Wa-Siha.
Lugha
ya Kichagga
Lugha ya Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana
na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo, Kimarangu, Ki-Old Moshi,Kikibosho, Kimachame, Kikirua na Kisiha. Lugha hizi zinakaribia kufanana
kulingana na jinsi makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Ki-Old Moshi
kinafanana na Kikirua, ambacho nacho kinafanana kidogo na Kimarangu. Vile vile
Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho.
Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha,
lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru
wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.
Historia
ya elimu kati ya Wachagga
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao
mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari
wa Kikristo
walijenga makanisa na shule. Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye
watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa
idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa
wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za
msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika
mikoa mingine Tanzania.
Shule nyingi za sekondari ziko
katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii
katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao
hapo. Hivyo wamishinari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za
wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3)
Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa
shule binafsi kama kitega-uchumi. Wakati wakazi wa mikoa mingine walisubiri
serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1,2 & 3 utagundua shule
katika mkoa Kilimanjaro vimezidi sana idadi ya shule katika miko mingine yote.
Ni vema pia kusema kwamba shule hizi
kuvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi wachagga tu.
Kilimo
na chakula
Wachagga hulima mazao ya chakula
kama vile mahindi,
maharagwe,viazi,
ndizi,
ulezi na mboga mbalimbali. Mazao ya
biashara kama vile kahawa,
nyanya
na vitunguu.
Ndizi
za Wachagga
Ingawa wachaga wa leo wanakula
vyakula mbali mbali kama vile ugali, wali
na viazi,
chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi. Kuna ndizi za aina mbalimbali na hutumika kwa matumiza
tofauti. Mfano ndizi kisukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu
kama tunda. Ndizi mshare kukatwa zikiwa mbichi na kupikwa chakula mbalimbali
pamoja na nyama ya ngombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage,
choroko,kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha
tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.
Aina nyingine ni ndizi-ngombe ambazo
huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa
kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.
Aina nyingine ni ndizi-mzuzu. Hizi
zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa
pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Darisalamu utaona ndizi- mzuzu
zikichomwa sambamba na muhogo au kuku-vumbi au kiti-moto.
Wachagga
na muhogo
Inasemekana kuwa "mchagga
halisi, hali muhogo
- akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa
wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila.
Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga
sumu ya sianidi ndani yao; watu waliozoea kutumia
mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa
muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani hasa wa Machame walifanya jaribio
bila kujua mbinu ya kuondoa sumu ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni
kwamba huko huko Kilimanjaro, majirani na watani wa wachagga yaani Wapare
walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.
Ulaji
kiti-moto
Pamoja na kilimo cha mazao, wachagga
hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo
kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na wachagga.
Ulaji wa "kiti moto" haukupendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar
es Salaam ambapo wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu
kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila
mengine na wasiyo waisalmu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa".
Majina
ya Kichagga
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia
huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano
familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi,Kimaro,
Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu,
Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi
na Vunjo. Kavishe,Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe,
Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri,
Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu
na Kilema. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario,
Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando,
Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka
Kibosho.Ukoo wa akina Teri wako Mamba Kiria na wachache Sango, Old Moshi na
wengine walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa Arusha.
Wachagga wengi hupenda kurudi
nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu.
Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo
kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao,
inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na
kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi
nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.
Utawala
wa jadi ya Wachagga
Watawala wa kichagga waliitwa
"Mangi". Hawa walihodhi mashamba, ngombe na waliheshimiwa kama
viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya
ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na
wakoloni (wajerumani), Mangi Sina wa kibosho - anajulikana kwa uhodari wake wa
vita katika kupigana na wamachame na kupora ngombe na mazao yao na Mangi
Marealle wa Marangu na Vunjo. Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia
mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya
kikoloni. Pia ndugu na watoto wa ma-Mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya
kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia
wanaaminika walikuwa ni kama mabepari wa kwanza wa ki-jadi, maana walifanyiwa kazi
na watu wengine wakati wao ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao. Usemi maarufu wa
"u-Mangi-meza" nadharia
inawezekana kuwa umetokana na
watawala hawa wa kichagga.
Ardhi
Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo
kwa watu wote, kwa wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha
mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi.
Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya
ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya
watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba
wa ardhi uchagani ulipelekea wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo
utakuta wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya nk wakiwa wamepanda
migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula. Ukienda kwenye mikoa
hii utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe
au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta katika makusanyio ya
wachaga mikoani mbali mbali.
Maoni
juu ya Wachagga
Ingawa wanaume wa kichagga
hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na
hufuga ngombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi
tabia hii imepungua miongon mwao. Wanawake wa kichagga (hasa kutoka Rombo) hujulikana
kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula.
Ingawa kipato cha wachaga ni kikubwa kulinganisha na cha makabila mengine,
takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa kuongoza kwa utapiamlo.
Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo kunatokana na wazazi kujali zaidi kazi
kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa wototo ni wale ambao wazazi wao ni
watu wapombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba uchagani kuna
vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa nibiashara kubwa.
Karibu kila kaya kumi natano kuna kila cha pombe na kiwango cha chini kabisa
cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya dede sita au lita
mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo Hii inawezekana kuwa
matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora.
Kuna sehemu nyingine za Uchaggani kama Old Moshi na Kibosho
ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi mchana na jioni. Sababu
nyingi ni kazi; mama wa kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hawana
desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani hivyo wanakuwa nyumbani
ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema
kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda
katika shuguli za kibiashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi
majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi.
Pia baadhi ya wamama wa kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni
ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri tofauti na
chakulawalichoandaliwa watoto japo ni chakula kilekile.pia wachaga wamekua na
desturi ya kuwaenzi wazee wao walio tangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa
pombe na nyama za mbuzi pale tu wanapo rudi nyumbani ifikapo mwezi desemba.
hili limekua ni swala la kawaida sana na halipingiki. wengi wao huwa wanarudi
na magari ndio sababu utaona ya kwambwa kila ifikapo mwezi desemba kila mwaka
foleni za magari zimekua zikiongezeka kutokana na wachaga kurudi nyumbani msimu
wa sikukuu. wengi wao wamekua wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya
nchi,Dj sek blog
No comments:
Post a Comment