MAHAKAMA
ya Hakim Mkazi wilaya ya Nzega mkoani Tabora imewahukumu watu watatu
kwenda Jela miaka 90 kwa kubainika na kosa la Unyanganyi wa kutumia silaha kuwapora Milioni 18 ambapo ni kinyume na kifungu cha 287 cha sheria ya kanuni ya adhabu.
Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi Silvester Kainda,
baada ya kusikiliza ushahidi wa mashitaka kwa washitakiwa watatu kati
ya watano,ushahidi umethibitisha bila kuacha shaka kuwa Antony
Joseph,Charles Richard na Samweli John wamehukumiwa kwenda jela miaka 90
huku kila mmoja akitumikia miaka 30 jela.
Awali ya hapo Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi mkaguzi msaidizi Mellito Ukongoji
aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo Aprili 2 mwaka 2013 watuhumiwa
watano waliotuhumiwa kwa kuteka wafanya biashara walio kuwa wakienda
mnadani Mambali na kupora milioni 18.
Ameiambia mahakama hiyo kuwa majambazi hayo yakitumia silaha aina ya Bunduki SMG 1 yalifanikiwa kupora fedha hizo za wafanya biashara.
Washitakiwa watatu kati ya watano wamekumbwa na hukumu hiyo ya miaka 90 jela ambao ni Antony Joseph, Charles Richard na Samweli John huku washitakiwa wawili wakiachwa huru baada ya kutobainika na hatia ya utekaji ambao ni Joseph Kisumo na Mkwangu Masaniwa.
Melito
ameiambia mahakama hiyo kuwa itoe adhabu kali ili iwefundisho kwao na
kwa jamii hata hivyo washitakiwa hao watatu walipewa nafasi ya kujitetea
hawakujitetea badala yake waliiomba mahakama hiyo iwapatie nakala ya hukumu zao.
No comments:
Post a Comment